Uncategorized

KOCHA YANGA AJITETEA ISHU YA UBAGUZI WA RANGI

admin July 27, 2020 3:47 pm


LUC Eymael aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa yeye sio mbaguzi ingekuwa hivyo asingeweza kufanya kazi ndani ya bara la Afrika kwa miaka mingi.

Leo, Eymael ametimuliwa kazi na mabosi wake Yanga kutokana na kitendo chake cha kutoa lugha zisizo za kiungwana zenye viashiria vya ubaguzi wa rangi kwa mashabiki wa Yanga kupitia sauti yake kwa vyombo vtya habari.

Kauli aliyoisema Eymael kuhusu mashabiki ni hii hapa:-“Sifurahii nchi hii (Tanzania). Nyinyi ni watu ambao hamjaelimika. Nimechukizwa. Sina gari, WiFi au DSTV. Mashabiki hawajui chochote kuhusu soka. Ni kama nyani au mbwa wanavyopiga kelele.”

Kuhusu ubaguzi wa rangi Eymael amesema:”Kama ningekuwa mimi ni mbaguzi wa rangi basi nisingeweza kufanya kazi miaka mingi Afrika, pia nisingeweka ishara ya kupinga ubaguzi na ndio maana jana nilipiga goti moja pale uwanjani,”.

JEMBE LA KAZI SIMBA FITI KUIVAA NAMUNGO FAINALI MWINYI ZAHERA AMCHANA EYMAEL, ATAJA MAKOSA YAKE MAKUBWA NDANI YA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply