Uncategorized

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

admin July 30, 2020 4:47 pm

HATIMA ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison raia wa Ghana itaamuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji.
Morrison ameingia katika mgogoro wa kimkataba na waajiri wake Yanga ambao wanadai ana mkataba wa miaka miwili huku mwenyewe akidai kuwa mkataba wake umefikia tamati hivi karibuni.
Uongozi wa Klabu ya Yanga umeamua kuliwasilisha suala hilo katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ili kuweza kupatia ufumbuzi wa mwisho.
Akizungumza na Championi Jumatano Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, amesema kuwa, suala la Morrison limefikishwa katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo italitolea ufafanuzi muda si mrefu.
“Yanga wamelifikisha suala la Morrison katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo ndiyo itakayotolea ufafanuzi suala hilo la mkataba wake ndani ya klabu hiyo.
“Kamati itakutana na kuamua juu ya suala hilo na itajua lini itatolea maamuzi suala hilo, taasisi ina utaratibu mzuri wa kutoa taarifa itakapotakiwa kutolewa, itatolewa kwa wakati, kwa sasa bado lipo ndani ya kamati,” alisema Ndimbo.
ALIYEFANIKISHA DILI LA SAMATTA KUKIPIGA ASTON VILLA APIGWA CHINI MAZIMA SIMBA YALIPIGIA HESABU KOMBE LA FA, KIKOSI CHATIA TIMU SUMBAWANGA LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply