Uncategorized

BAADA YA KUSEPA NA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR, MSERBIA ATOA LA MOYONI

admin September 20, 2020 6:47 am


 ZLATKO Krmpotic, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakijitahidi kufanya vizuri ndani ya uwanja jambo ambalo limempa matumaini ya kuendelea na kasi yake ya ushindi kwenye mechi zake zijazo.

Yanga jana Septemba 19 ilisepa na pointi tatu mazima mbele ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba kwa ushindi wa bao 1-0 na kuifanya ifikishe pointi saba ikiwa nafasi ya kwanza Kwenye msimamo.

Bao la ushindi lilipachikwa kimiani na Tonombe Mukoko akimalizia pasi mpenyezo ya Tuisila Kisinda ndani ya 18 iliyowashinda mabeki wa Kagera Sugar.

Krmpotic raia wa Serbia amesema:”Ninaona kuna kitu ambacho kipo kwa wachezaji kila siku wanabadilika na kufanya kile ambacho ninawaambia hilo kwangu ni furaha.

“Kiukweli mchezo wetu mbele ya Kagera Sugar haukuwa mwepesi katika hili nawapongeza wapinzani wangu lakini kwa kuwa tumepata pointi tatu basi mengine yatafuata,” amesema.

Baada ya mechi ya jana, mashabiki wa Yanga wanachama na wapenzi wa klabu wa mkoa wa Kagera walipata chakula cha usiku ikiwa ni wachezaji pamoja na viongozi ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa furaha.

SIMBA V BIASHARA UNITED KUKIWASHA LEO KWA MKAPA, REKODI HIZI ZINAONGEA HASSAN KESSY KAMILI KUKUTANA NA MUZIKI WA SARPONG

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply