Uncategorized

MTIBWA SUGAR YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA

admin September 21, 2020 10:47 am


 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa unajipanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Yanga utakaopigwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Yanga itamenyana na Mtibwa Sugar ikiwa imetoka kushinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wao uliochezwa Septemba 19, Uwanja wa Kaitaba.

Inakutana na Mtibwa Sugar ambayo nayo imetoka kushinda mbele ya Ihefu FC kwa bao 1-0 Uwanja wa Sokoine, Septemba 18.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema kuwa wapo tayari kumenyana na Yanga wanahitaji kupata pointi tatu muhimu.

“Ushindi ndio kitu ambacho tunakihitaji hakuna jambo jingine. Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini wasitarajie kupata wepesi kwetu tutapambana kushinda,” alisema Kifaru.

KAGERA SUGAR MAJANGA MATUPU, DAKIKA 270 BILA POINTI KIBINDONI HESABU ZA YANGA ZIPO NAMNA HII KUELEKEA MCHEZO WAO DHIDI YA MTIBWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply