Uncategorized

SIMBA KUSHUKA UWANJANI KESHO KUMENYANA NA AFRICAN LYON

admin September 21, 2020 6:48 pm


 KIKOSI cha Simba kesho, Septemba 21 kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza kwa ajili ya kuwapa nafasi wachezaji ambao hawajacheza mechi za ushindani kuwa fiti.


Pia mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Gwambina FC ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 10:00 jioni ambapo kiingilio ni buku tatu mzunguko na buku tano kwa VIP. Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa mashabiki ni muhimu kujitokeza kuendelea kuipa sapoti timu yao.


“Natambua kwamba mashabiki wanaipenda timu yao ndio maana tumeona kwamba viingilio viwe ile kiasi chake kwenye mechi zetu za ligi pia lakini ninawaomba mjitokeze kwa wingi  kuipa sapoti timu yenu.


“Malengo ya mchezo huu ni kwa ajili ya kuwapa uimara wachezaji wetu hasa wale ambao walikosa kucheza mechi za hivi karibuni ili kwenda sawa na kasi ya ushindani.


“Huu ni mpango wa Kocha Mkuu, (Sven Vandenbroeck) katika kuimarisha kikosi hivyo mashabiki endeleeni kuipa sapoti timu bila kuchoka,” amesema. 


Baada ya jana Septemba 20 kumalizana na Biashara United kwa ushindi wa mabao 4-0 mchezo wa Simba unaofuata ni Septemba 26 Uwanja wa Mkapa dhidi ya Gwambina FC.

GWAMBINA YAYEYUSHA POINTI TATU MBELE YA RUVU SHOOTING WALIOIMALIZA MBEYA CITY JANA LEO WAWEKWA KANDO NDANI YA AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply