Uncategorized

ISHU YA DUKA LA JEZI SIMBA WAIJIBU YANGA, WATAJA WASHINDANI WAO NI WAARABU

admin September 24, 2020 3:47 pm


 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo kwa sasa ni kushindana na timu kubwa ndani ya Afrika huku ukisema kuwa masuala mengi ambayo yamefanywa na watani zao wa jadi, Yanga walishayafanya wao pia nyuma.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameyasema hayo leo Septemba 24 alipofanya ziara ndani ya Global Group ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra alipokuwa akizungumza na Watanzania kupitia +255 Global Radio.


Manara amesema“Walichokifanya Yanga SC kuhusu kufungua duka la jezi sisi tulishafanya miaka minne iliyopita, sisi tuna malengo makubwa sasa hivi na tuko mbali sana, duka sio ishu kwetu.

 

“Sisi tunashindana na Al Ahly na Casablanca FC kwenye mitandao ya kijamii, unatulinganishaje na Yanga SC? Chukua akaunti yetu ya Instagram, linganisha na ya kwao, chukua akaunti yao rasmi, viongozi na akaunti za wachezaji wao hawatufikii.” 

ISHU YA CHAMA KUIBUKIA YANGA, UONGOZI WA SIMBA WAJIBU NAMNA HII AZAM FC KITAMBO WALITIA TIMU AL AHLY, CORONA YATIBUA WAO KUTUA REAL MADRID

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply