Uncategorized

SAMATTA AIBUKIA UTURUKI DILI LA MIAKA MINNE

admin September 25, 2020 8:47 am


MSHAMBULIAJI wa timu ya soka nchini Tanzania Mbwana Samatta amejiunga na klabu ya Uturuki Fenerbahce kwa mkataba wa miaka minne.

Samatta alikuwa anakipiga ndani ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England, ila kwa msimu wa 2020/21 alikwama kupenya kikosi cha kwanza kutokana na kushindwa kuonyesha makeke aliyokuwa nayo awali.


Aliibukia ndani ya Aston Villa akitokea Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji na ni mtazania wa kwanza kucheza Ligi Kuu England ambayo ni namba moja kwa kufuatiliwa duniani.


Akiwa ndani ya Villa, Samatta aliweza kutupia mabao mawili na timu yake ilikuwa kwenye hatihati ya kushuka daraja ila iliponea kwenye tundu la sindano baada ya kushinda mchezo wake wa mwisho.

POLISI TANZANIA YAZITAKA POINTI TATU ZA DODOMA FC, MMOJA KUUKOSA MCHEZO YANGA YAZIFUATA POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR LEO, MORO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply