Uncategorized

RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO OKTOBA 22, YANGA NA SIMBA KAZINI

admin October 22, 2020 5:47 am


 LEO Oktoba 22, Ligi Kuu Bara inaendelea ambapo timu nne zitakuwa kwenye viwanja viwili tofauti kusaka pointi tatu muhimu.


Yanga itakuwa Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni kumenyana na Polisi Tanzania mchezo wa ligi. Timu ya Polisi Tanzania imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Gwambina FC mchezo wao uliopita huku Yanga ikitoka kushinda mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union mchezo wao wa mwisho wa ligi.


Tanzania Prisons itaikaribisha Simba, Uwanja wa Nelson Mandela saa 10:00 jioni, Prisons imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania na Simba mchezo wake wa mwisho ilishinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania.

TANZANIA PRISONS: TUMEWAFUNGA MARA NYINGI SIMBA, TUTAWAFUNGA TENA MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply