Uncategorized

HIMID MAO KAZI INAENDELEA,KILA KITU KINAWEZEKANA

admin October 24, 2020 2:47 pm


 HIMID Mao mzawa anayekipiga ndani ya Klabu ya ENPPI ya Misri amesema kuwa kwa namna soka la Tanzania linavyokuwa kwa kasi ni rahisi kwa wachezaji wengi wazawa kupata timu nje ya nchi.


Himid ambaye pia aliitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Burundi amesema kuwa anafurahi kuona ushindani ndani ya Bongo unavyozidi kuwa mkubwa.

Aliibuka nchini Misri akitokea Klabu ya Azam FC ambayo leo imeibukia Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaochezwa Oktoba 26, Uwanja wa Jamhuri, Moro.

Himid amesema:”Kwa namna ambavyo mambo yanakwenda ndani ya Bongo ninaona kwamba ushindani unazidi kuwa mkubwa na wachezaji wanajituma.

“Muhimu kuona kila mtu anatimiza ndoto zake na kupata fursa ya kufanya kile ambacho anakipenda inawezekana.”
ORODHA YA WACHEZAJI 22 WA AZAM FC WALIOANZA SAFARI KUIBUKIA MOROGORO YANGA WAPEWA ONYO MAPEMA KABISA BAADA YA KUSHINDA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply