Uncategorized

KAGERA SUGAR: TUTARUDI KWENYE UBORA WETU, MASHABIKI WATUPE SAPOTI

admin October 29, 2020 9:47 am


NYOTA wa Kagera Sugar, Yusuph Mhilu amesema kuwa anaamini timu yake ya Kagera Sugar itarejea kwenye ubora wake na itafanya vizuri katika mechi zao zijazo licha ya kuwa na mwendo wa kusuasua kwa msimu wa 2020/21.


Kwa sasa Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Mecky Maxime ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 5 baada ya kucheza mechi nane.

Safu ya ushambuliaji imefunga mabao matano na kinara ni Mhilu akiwa nayo mabao matatu ambayo aliwafunga Azam FC, KMC na Namungo FC.


“Bado kuna nafasi ya timu kurejea kwenye ubora wake, makosa ambayo yamepita ninaamini kwamba benchi la ufundi litayafanyia kazi nasi tutafanya vizuri kikubwa mashabiki watupe sapoti,” amesema.


Mchezo unaofuata kwa Kagera Sugar ni dhidi ya Mtibwa Sugar itakuwa Novemba Mosi, Uwanja wa Kaitaba.


Inakutana na Mtibwa Sugar ambayo imetoka kushinda mbele ya Azam FC kwa kuifunga bao 1-0 ipo nafasi ya 10 na pointi zake 11 baada ya kucheza mechi 8.

YANGA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA BIASHARA UNITED AZAM FC AKILI ZOTE KWA JKT TANZANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply