Uncategorized

KASHASHA: CHAMA ATAWASAIDIA YANGA KUTOKANA NA UBORA

admin November 11, 2020 7:47 am

 


MTANGAZAJI na mchambuzi maarufu wa masuala ya michezo nchini, Alex Kashasha ‘Mwalimu Kashasha’, amekiri kuwa kama Yanga itafanikiwa kumsajili kiungo nyota wa Klabu ya Simba, Clatous Chama,basi atawasaidia Yanga kutokana na ubora alionao.

 

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazomhusisha kiungo huyo wa Simba kuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga ili kujiunga na timu hiyo.

 

Akizungumza katika mahojiano maluum ya +255 Global radio yaliyoruka mubashara kupitia Global TV Online, Kashasha amesema: “Kama ni kweli Yanga watafanikisha usajili wa Chama kama ambavyo tetesi zimekuwa zikieleza, basi utakuwa usajili bora, na naamini atakuwa msaada mkubwa kwao.


“Miongoni mwa wachezaji bora na wenye nidhamu ni Chama, uwezo wake ndani ya uwanja umekuwa ukionekana hivyo nguvu zake zikiongezwa ndani ya Yanga basi timu hiyo itafanya vizuri kwenye mashindano itakayoshiriki,” amesema.


SIMBA YATOA TAMKO ISHU YA CHAMA KUIBUKIA YANGA POCHETTINO ATAJWA KUIBUKIA ATHLETIC BILBAO KUBEBA MIKOBA YA GARITANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply