Uncategorized

PIALALI AMSHINDA MFILIPINO KWA POINTI

admin November 29, 2020 11:47 am


 BONDIA Iddi Pialali wa Bagamoyo Pwani hapa nchini, leo alfajili amefanikiwa kumtwanga Bondia wa Kimataifa Arnel Tinampay kutoka Ufilipino.

Tinampay alikubali kichapo hicho kwenye pambano la raundi nane lililopigwa Ukumbi wa Next Door Arena uliopo Masaki Jijini Dar.


Katika pambao hilo mabondia wote walianza kushambuliana kwa kasi kila mmoja akionekana kutaka kumlaza mwenzake kwa KO lakini kutokana na umahiri waliouonesha walijikuta wote wakimaliza raundi zote nane.


Wawili hao baada ya kumaliza pointi hizo majaji wa mpambano huo walimpa ushindi Pialali kufuatia kumtwanga ngumi Mfilipino huyo na kutaka kumuangusha mara kadhaa hali iliyopelekea aonekane kujikongoja ilimradi amalize pambano hilo.

SVEN ATOA NENO KIMATAAIFA, RAMANI IMECHORWA NAMNA HII BERNARD MORRISON AAHIDI MABAO KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply