Uncategorized

MTIBWA SUGAR YAINYOOSHA KMC JAMHURI, MOROGORO

admin December 11, 2020 3:47 pm

 


KIKOSI cha Mtibwa Sugar leo Desemba 11 kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri,Morogoro. 

Bao pekee la ushindi limepachikwa na Salum Kihimbwa dakika ya 21 kwa kichwa akimalizia pasi ya Kanoni aliyamwaga majalo kutoka pembeni mwa uwanja.


Licha ya jitihada za KMC kupambana kupitia nyota wao Relliants Lusajo na Emmanuel Mvuyekure kupata bao la kusawazisha milango ilikuwa migumu.


Shukrani kwa Wanamtibwa zimfikie Abutwalib Mshery mlinda mlango namba moja wa timu hiyo ambaye alisimama imara kuokoa hatari zote.


Kihimbwa amesema kuwa walipata nafasi nyingi kwenye mchezo huo ila walishindwa kuzitumia licha ya kupata pointi tatu muhimu. 


Juma Kaseja,  nahodha wa KMC ambaye ni kipa namba moja amesema kuwa makosa ambayo wamefanya yamewaponza wapoteze pointi tatu kwenye mchezo huo.

KIUNGO ALIYEWAVURUGAVURUGA SIMBA AKUBALI KUTUA YANGA MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply