Uncategorized

NYOTA WATATU WASEPA NDANI YA AZAM FC

admin December 20, 2020 11:47 am


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa nyota wake Alain Thiery Akono Akono amepata dili la kwenda Malysia baada ya mabosi wa timu hiyo kuvutiwa na uwezo wake.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabiti amesema kuwa kila kitu kikiwa wazi ataweka sawa na mashabiki watajua ni timu ipi anakwenda.


Akono anakuwa ni nyota wa tatu kusepa ndani ya kikosi cha Azam FC na kuibukia kwenye timu nyingine kupata changamoto mpya.

“Mazungumzo na kila kitu kuhusu usajili wa Ankono Akono yamekwenda sawa na kinachotakiwa ni mashabiki kuwa na subira ili kupata taarifa kamili ambazo tutazitoa hivi karibuni, ila ukweli ni kwamba amepata timu Malysia” .


Akono anakuwa ni mchezaji wa tatu kuuzwa kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Klabu ya Azam FC wengine ni pamoja na Novartus Dismas ambaye yupo Israel na Shaban Chilunda yupo zake nchini Morroco.

JKT TANZANIA YASIMAMISHA USAJILI WA KMC BENCHI LA UFUNDI SIMBA LAFANYA ZIARA UWANJA WATAKAOSAKA USHINDI JUMATANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply