Uncategorized

THOMAS ULIMWENGU AREJESHA SHUKRAN KWA WATANZANIA

admin January 7, 2021 5:47 am

 


THOMAS Ulimwengu Mtanzania anayekipiga ndani ya Klabu ya TP Mazembe amewashukuru mashabiki wa Tanzania kwa sapoti zao pamoja na pongezi ambazo wamemtumia baada ya kutimiza majukumu vema akiwa na timu hiyo.


Jana, Januari 6 wakati TP Mazembe ya Congo ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Bouenguidi alikuwa miongoni mwa washambuliaji waliopeleka kilio kwa wapinzani hao mapema.


Dakika ya 14 alipachika bao la kuongoza ambalo liliwapa nguvu Mazembe walipachika bao la pili dakika ya 45 na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0 wakiwa Uwanja wa Stade TP Mazembe.


Kipindi cha pili wapinzani wao Bouenguidi walipata bao la kufuta machozi dakika ya 79 kupitia kwa Djoe Dayan Boussougou ila halikuweza kuwapa faida wapinzani hao kusong mbele hivyo watashiriki Kombe la Shirikisho. 


Ulimwengu amesema:”Shukran sana kwa wote ambao wapo pamoja nami na wananifuatilia law dua zao,” .

SIMBA KUIBUKA ZANZIBAR NA MAJEMBE MAWILI YA KAZI BEKI ALIYEKATALIWA NDANI YA SIMBA AWAUMBUA MABOSI ZAKE AKIWA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply