Simba SC

YANGA YATAMBIA UBINGWA LIGI KUU, SIMBA KIMATAIFA

admin January 17, 2021 6:47 pm


DIRISHA la usajili lilifungwa rasmi Ijumaa usiku na kushuhudia timu za Simba na Yanga zikishusha wachezaji wapya na kuwatambulisha ikiwa umebaki muda mchache kabla ya dirisha hilo kufungwa.

Yanga ilifunga usajili wao kwa kuutambulisha usajili wa mshambuliaji wao mpya mwenye uraia wa Burundi, Fiston Abdoul Razak huku Simba wao wakimaliza na kiungo mshambuliaji raia wa Zimbwambwe Tatenda Perfect Chikwende.

Kutokana na sajili hizo viongozi wa pande zote mbili wameibuka huku kila upande ukijinasibu kuwa kwenye mawindo yake Simba ikijinasibu kwenda kimataifa huku Yanga wao wakitamba kusepa na kombe la Ligi Kuu.

Mjumbe wa kamati ya usajili wa Yanga Injinia Hersi Said yeye amesema: “Tumekamilisha usajili wa maboresho ndani ya dirisha dogo la usajili kwa lengo la kuushinda kombe la Ligi Kuu msimu huu,”

Kwa upande wa Simba Ofisa mtendaji mkuu (CEO) wa timu hiyo Barbara Gonzalez yeye amesema kuwa “Usajili wa Perfect Chikwende ni kwa ajili ya kuiongezea nguvu timu yetu katika safu ya ushambuliaji kuelekea katika michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika ambayo tumetinga hatua ya Makundi,”

NDAYIRAGIJE MATUMAINI KAMA YOTE MBELE YA CHIPOLOPOLO MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply