Yanga SC

YANGA WAREJESHA KWA JAMII,GHANA NA BONGO

admin January 25, 2021 11:47 am

 


MICHAEL Sarpong mshambuliaji ndani ya kikosi cha Yanga alipata nafasi ya kutoa msaada kwenye kituo cha Royal Seed Orphanage kilichopo nchini Ghana wiki hii.

Sarpong alirejea Ghana, Januari 13 baada ya kumaliza kazi ya kusaka Kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar.

Ndani ya Ligi Kuu Bara ametupia mabao manne wakati timu yake ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo na anatarajiwa kurejea leo kujiunga na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

Pia nyota mwingine ambaye alifanya kama Sarpong kwa kurejesha kwa jamii ni Mukoko Tonombe ambaye yeye jana Januari 24 alitembelea kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni, Mkwajuni.

SIMBA YAFUNGUKIA SUALA LA ZAHERA KUWA KWENYE BENCHI LA UFUNDI TAIFA STARS HESABU ZOTE KWA GUINEA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply