Ligi Kuu

MASAKA, OPAH WANAUTAKA UFALME WA FATUMA

admin February 3, 2021 12:47 pm

 


KASI ya washambuliaji Opah Clement wa Simba Queens na Aisha Masaka wa klabu ya Yanga Princess kwenye Ligi Kuu ya Wanawake, inaashiria wazi kuwa nyota hao wamejipanga kuumaliza ufalme wa mshambuliaji wa JKT Queens Fatuma Mustapha katika vita ya ufungaji bora msimu huu.

Mabao saba aliyoyafunga Opah kwenye mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza dhidi ya TSC Queens yamemfanya afikishe mabao 20 na kumfikia Fatuma aliyekuwa akiongoza chati ya wafungaji, huku Masaka yeye akiwa tayari ameweka kambani mabao 15.

Akizungumzia malengo yake Masaka amesema : “Kwanza najisikia furaha kuwa sehemu ya kikosi cha klabu ya Yanga na kwa kuanza vizuri msimu huu kwa kufunga mabao 15 mpaka sasa, malengo yangu ni kupambana kuisaidia Yanga kuibuka na ubingwa msimu huu, lakini kama mshambuliaji nataka pia kuibuka na tuzo ya ufungaji bora,”

MFAUME MFAUME ATAJA KILICHOMPA USHINDI CLASS KMC KAZINI KESHO MBELE YA NAMUNGO FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply