epl

LEO NI VITA YA KIBABE LIGI KUU ENGLAND, CHELSEA V MANCHESTER UNITED

admin February 28, 2021 9:47 am


 UWANJA wa Stamford Bridge leo Februari 28 majira ya saa 1:30 utachezwa mchezo mkali wa Ligi Kuu England ambao unatarajiwa kuwa mkali mwanzo mwisho.

Ni Thomas Tuchel Kocha Mkuu wa Chelsea ambaye atamkaribisha ndugu yake Ole Gunnar Solskjaer wa Manchester United.

Tambo kwa makocha wote wawili zimetawala ambapo kila mmoja ameweka wazi kwamba anahitaji pointi tatu muhimu.

Kocha wa Chelsea amesema:”Kwenye kila mchezo kwetu tunahitaji ushindi na tuna amini kwamba na washindani wetu wanahitaji ushindi hivyo tutapambana muda wote,”.


Kocha wa Manchester United Ole amesema:”Ni ngumu kusema kwamba hatuhitaji ushindi ndani ya uwanja, tutapambana ili kupata matokeo mazuri,”.

Tuchel atakosa huduma ya beki mkongwe, Thiago Silva huku United wao nyota wao Paul Pogba, Edinson Cavani hawa ni majeruhi.

 Kwenye msimamo Chelsea ipo nafasi ya tano na pointi zake ni 43 inakutana na United iliyo nafasi ya pili na pointi zake 49.

IBRAHIM AJIBU AAMBIWA AONGEZE JUHUDI NDANI YA UWANJA JURGEN KLOPP ATAJWA KUIBUKIA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply