epl

CITY YAMPIGA MTU MKONO

admin March 12, 2021 7:47 am

 


UWANJA wa Etihad ulikusanya jumla ya mabao 7 baada ya dakika 90 kukamilika Kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliowakutanisha Manchester City v Southampton. 


Ubao ulisoma Manchester City 5-2 Southampton. Kevin De Bruyne alifungua akaunti ya mabao dakika 15 na 59, Riyad Mahrez alifunga dakika ya 40 na 55 na bao moja ni mali ya Gundogan ilikuwa nj dakika ya 45+3.


Mabao ya Southampton yalipachikwa kimiani na James Ward-Prowse dakika ya 25 kwa penalti na Che Adams dakika ya 56 yaliwawafanya waache pointi tatu mazima ugenini.


City ya Pep Guardiola inajikita kileleni ikiwa na jumla ya pointi 68 baada ya kucheza jumla ya mechi 29 huku Southampton ikiwa nafasi ya 14 na pointi zake 33 imecheza jumla ya mechi 28.

GOMES WA SIMBA BADO ANAIFIKIRIA YANGA MAGUIRE AGOMA KUOMBA MSAMAHA, ASEMA YEYE NI BEKI SIO MSHAMBULIAJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply