Simba SC

MANULA AINGIA ANGA ZA MAMELODI SUNDOWNS

admin April 12, 2021 5:47 am




KIPA namba moja wa Simba, Aishi Manula inaelezwa kuwa amewekwa kwenye anga za timu kubwa za Afrika Kusini pamoja na Sudan ambazo zinahitaji kupata saini yake.

Manula amekuwa kwenye ubora ndani ya uwanja baada ya kuwa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kimetinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwenye mechi sita za hatua ya makundi alikaa langoni kwenye mechi tano huku lango lake likiwa salama kwenye mechi tatu ilikuwa AS Vita 0-1 Simba, Simba 1-0 Al Ahly na Simba 3-0 Al Merrikh. Alitunguliwa mechi mbili ilikuwa Simba 4-1 AS Vita na Al Ahly 1-0 Simba.

Mechi moja dhidi ya Al Merrikh ugenini alikaa langoni kipa namba mbili Beno Kakolanya naye aliyeyusha dakika 90 bila kufungwa.

Kutokana na uwezo wa Manula habari zinaeleza kuwa Al Merrikh ya Sudan pamoja na Mamelodi Sundowns nao wanahitaji saini yake.

Kuhusu hilo Manula amesema kuwa kwake ni furaha kuhitajika na timu mbalimbali ila bado ana mkataba na mabosi wake Simba.

YANGA: TUTAFANYA VIZURI NAFASI IPO MANCHESTER UNITED YAPINDUA MEZA KIBABE MBELE YA TOTTENHAM

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply