Azam FC

AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA JKT TANZANIA

admin April 14, 2021 4:47 am


VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 16 Uwanja wa Jamhuri Dodoma, utachezwa saa 8:00 mchana.

Bahati amesema maandalizi yanakwenda vizuri na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ujao na maandalizi yanakwenda sawa hivyo ni suala la kusubiri na kuona.

“Ushindi ni jambo ambalo tunalihitaji hivyo kwa morali ambayo wanayo wachezaji tunaamini kwamba tutafanya vizuri,” .

Kwenye msimamo wa ligi, Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 25 ina pointi 47 inakutana na JKT Tanzania yenye pointi 27 ipo nafasi ya 12.

SIMBA: MTIBWA SUGAR HUWA WANATUPA CHANGAMOTO, GWAMBINA YATUMA SALAMU ZAKE KMC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply