epl

AUBA NA LACAZETTE WA ARSENAL HATIHATI KUIKOSA EVERTON LEO

admin April 23, 2021 4:48 am


 KIKOSI cha Arsenal ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta leo kinatarajia kuwakosa nyota wake wawili tegemeo kutokana na sababu mbalimbali.

Mchezo wa leo ambao ni wa Ligi Kuu England unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Emirates kwa wababe hao kusaka pointi tatu.

Pierre Aubameyang ambaye ni nahodha huyu anasumbuliwa na Malaria hivyo bado hajawa fiti kwa ajili ya kuendelea kuipambania timu yake licha ya kwamba anaendelea vizuri.

Auba alipata Malaria wakati alipokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Gabon.

Mwingine ni Alexandre Lacazette mwenye mabao sita ambaye aliumia nyama za paja na huenda akaukosa pia mchezo ujao dhidi ya Villarreal.

AZAM FC BADO WAKOMALIA JAMBO LAO KIGOGO WA SUPER LEAGUE AKOMAA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply