Simba SC

VINARA WA LIGI KUU BARA WATUA DAR NA POINTI TISA ZA KANDA YA ZIWA

admin April 25, 2021 1:48 pm


 BAADA ya kikosi cha Simba kukusanya pointi zake 9 kanda ya ziwa kimerejea Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mechi zake za Ligi Kuu Bara. 

Ikiwa ipo nafasi ya kwanza na pointi 58 inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji, Aprili 27, Uwanja wa Mkapa.

Ilianza ziara ya kanda ya ziwa Aprili 18 ambapo ubao ulisoma Mwadui 0-1 Simba, Kagera Sugar 0-2 Simba, Aprili 21 na Gwambina FC 0-1 Simba Aprili 24.

Bao pekee la ushindi la Mohamed Hussein liliweza kuishusha Yanga nafasi ya kwanza na kuwapeleka nafasi ya pili wakiwa na pointi 57.

Simba imecheza jumla ya mechi 24 na Yanga imecheza jumla ya mechi 26 ndani ya ligi kwa msimu huu wa 2020/21 ambao una ushindani mkubwa.

YANGA V AZAM FC KWA MKAPA LEO KITAUMANA MANE NA SALAH WAAMBIWA KWAMBA SIO WASHAMBULIAJI HALISI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply