Simba SC

PATRICK AUSSEMS AIPA NAFASI SIMBA KUTINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

admin May 1, 2021 11:47 am


  Kocha wa zamani wa Simba SC, PATRICK Aussems ameibuka na kusema kuwa Simba SC ina nafasi kubwa ya kuweza kufika fainali katika michuano hiyo kutokana na kurekebisha mambo mengi aliyoshauri wakati yupo ndani ya timu hiyo.

 

Aussems ambaye kwa sasa ni kocha wa AFC Leopards ya Kenya licha ya kuwa kwenye mapumziko nchini Ufaransa baada ya Ligi ya Kenya kusimama kutokana na kuwepo kwa ‘lockdown’ ya Corona, aliondoka Simba mwaka 2019 baada ya kutimuliwa kutokana na mwenendo mbaya wa timu


Aussems amesema kuwa Simba ya sasa imebadilika kutokana na kukamilisha miondombinu yake, hivyo inaweza kufanya chochote tofauti na wakati wake alipokuwa kwenye timu hiyo.

 

“Unajua wakati ule Simba haikuwa na miondombinu mizuri wala uwanja wake wa mazoezi kwa sababu tulikuwa tukifanya mazoezi katika viwanja vya watu wakati mwingine Uwanja wa Boko na wakati mwingine Uhuru tena ikiwa ni kwa kusubiri wenye timu zao wamalize kwanza.

 

“Lakini sasa Simba inamiliki kila kitu kama zilivyo timu nyingine kubwa Afrika ndiyo maana inaweza kufanya vyema katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ubora ambao inaonyesha naona wanayo nafasi kubwa ya kucheza fainali kwa kuwa ni timu ambayo imepiga hatua kubwa,” alisema Aussems.


Simba imepangwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambapo inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza ugenini kati ya Mei 14-15 na mchezo wa marudio itakuwa ni Uwanja wa Mkapa.


Chanzo:Championi

JURGEN KLOPP: MAISHA NI MAFUPI SANA, HANA HOFU NA MANCHESTER AJIBU, GADIEL BYE BYE SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply