Yanga SC

ISHU YA LAMINE KUDAI KUWA ANADAI MKWANJA IPO HIVI

admin May 20, 2021 5:47 am

 IMEELEZWA kuwa taarifa zinazoeleza kuwa nahodha wa Yanga, Lamine Moro anadai mshahara wake hazina ukweli.

Nyota huyo alisimamishwa na Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi Mei 15 kwa kueleza kuwa hakuwa na nidhamu kwa kushindwa kufuata taratibu ambazo zimewekwa na kocha huyo jambo lililolazimu arudishwe kutoka Mtwara.

Alikosekana kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa ambapo dakika 90 ubao ulisoma Namungo 0-0 Yanga na nahodha alikuwa mshikaji wake Bakari Mwamnyeto.

Pia jana Mei 19 alikosekana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania ambapo Yanga walishinda mabao 2-0 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Taarifa hiyo imeeleza:”Lamine hadai kitu ndani ya Yanga hakuna fedha ambazo anadai hivyo hizo taarifa za kwamba anadai fedha ni uongo,”.

Ofisa Habri wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa nidhamu ni jambo linalozingatiwa ndani ya Yanga.

Hivi karibuni Habari zilieleza kuwa Lamine alidai mshahara jambo lililopelekea ashindwe kufuata utaratibu uliowekwa.

AZAM FC KAMILI GADO KUIVAA BIASHARA UNITED LEO KUMBE INJINIA HUVAA JEZI YA KAIZER CHIEFS AKIWA NA FURAHA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply