Simba SC

SABABU ZA SIMBA KUSHINDWA KUIFUNGA KAIZER CHIEFS DAR

admin May 20, 2021 6:47 am

 UONGOZI wa Simba umesema kuwa ikiwa wachezaji hawatajitoa  katika mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs utakaochezwa Uwanja wa Mkapa itakuwa ngumu kwao kushinda.

Simba ina kibarua cha kusaka ushindi wa mabao zaidi ya matano katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 22. 

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa FNB Soccer City,  Simba ilishuhudia ubao ukisoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanaweza kufanya kila kitu na kuahidi fedha ndefu ila wachezaji wasipoamua hawatashinda.

“Ikiwa tutafanya kila kitu kwa ajili ya mchezo wetu na tukawekeza kwa asilimia kubwa kama wachezaji hawataamua kujituma na kufanya kweli basi itakuwa ngumu kwetu kushinda.

“Wachezaji wana jukumu la kujitoa zaidi ya asilimia 100 na zaidi katika kusaka ushindi na tunaamini kwamba inawezekana. Mchezo wetu wa mwanzo ugenini tulimiki mpira sawa nakubali lakini hatujashinda,” amesema Manara.

KUMBE INJINIA HUVAA JEZI YA KAIZER CHIEFS AKIWA NA FURAHA YANGA YAENDELEA KUNG’ANG’ANIA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply