Yanga SC

YANGA YAWAITA MASHABIKI AZAM COMPLEX

admin June 3, 2021 12:47 pm


UONGOZI wa Yanga umewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti kubwa timu yao katika mchezo wao wa kirafiki unaotarajiwa kuchezwa Juni 6 saa 1:00 usiku.

Mchezo huo utakuwa wa kirafiki ikiwa  ni lengo la Kocha Mkuu,  Nassreddine Nabi kuwaimarisha  wachezaji wake ambapo watamenyana na African Lyon. 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mashabiki wajitokeze kuipa sapoti timu yao.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao kwani tuna mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon utachezwa Uwanja wa Azam Complex, ” amesema. 

Kiingilio katika mchezo huo mzunguko ni 3,000 na VIP ni 5,000.

KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA RUVU SHOOTING LEO LIVE: RAIS WA TFF, WALLACE KARIA ANAZUNGUMZA NDANI ya GLOBAL RADIO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply