Simba SC

KUMBE! SIMBA WANGETULIA WANGEWAFUNGA KMC MABAO MENGI

admin July 13, 2021 6:47 am


 NAHODHA wa KMC, Juma Kaseja ambaye alikaa langoni Julai 7 na kuokota mabao mawili yaliyofungwa na Chris Mugalu amesema kuwa wapinzani wao wangetulia Simba wangewafunga mabao mengi kipindi cha kwanza.

Kaseja ambaye ni Tanzania One aliweka wazi kwamba kwenye mchezo huo wa ligi wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma KMC 0-2 Simba, timu yao ilifanya makosa mengi kipindi cha kwanza.

Kipindi cha kwanza tulifanya makosa mengi sana na kama wapinzani wetu wangekuwa makini kwa nafasi ambazo walizipata basi wangetufunga mabao mengi kwa kutumia makosa yetu.

“Lakini kipindi cha pili ilikuwa ngumu kwao kutufunga kwa kuwa makosa ambayo tulifanya kipindi cha kwanza tulifanyia kazi hivyo walishindwa kutufunga, nasi tulishinwa kuwafunga,” amesema.

Kocha Msaidizi wa KMC, Habib Kondo amesema kuwa walifungwa kwa kuwa walishindwa kutengeneza nafasi jambo ambalo watalifanyia kazi kwenye mechi zao mbili zilizobaki.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE BREAKING: BODI YA LIGI YATANGAZA SIKU YA SIMBA KUKABIDHIWA UBINGWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply