Simba SC

BERNARD MORRISON AKABIDHIWA TUZO YA MCHEZAJI BORA

admin July 27, 2021 2:44 pm


 KIUNGO Mshambuliaji wa Simba raia wa Ghana, Bernard Morrison, amekabidhiwa kitita cha shilingi Ml 1, kutoka kampuni ya Emirate Alluminium baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Mwezi Juni.

Nyota huyo mzee wa kuchetua ametwaa tuzo hiyo baada ya kura za mashabiki kupigwa kwa wingi kupitia mitandao ya kijamii.

Alitwaa tuzo huyo baada ya kuwashinda wachezaji wenzake ambao ni Luis Miquissone na nahodha wake John Bocco, ambapo walikuwa wakiwania tuzo hiyo pamoja.

 

Tuzo hiyo imekuwa ikitolewa na Kampuni ya Emirate Alluminum kila mwezi, huku mchakato wa kumpata mshindi huendeshwa na Simba kupitia kura za mashabiki wa klabu hiyo.

SportPesa YAIPA MILIONI 100 SIMBA KISA  KESI YA MORRISON, YANGA WATAMBA KUIPORA SIMBA UBINGWA WA VPL NA FA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply