KMC FC

NYOTA WA SIMBA SHEVA KUIBUKIA KMC

admin August 17, 2021 11:45 am


 TAARIFA kutoka kambi ya KMC, zinasema kuwa klabu hiyo ipo mbioni kukamilisha usajili  wa mshambuliaji wa Simba, Miraji Athuman ‘Sheva’.

 

Mtoa taarifa huyo anasema kuwa KMC wanamtaka mchezaji huyo ili kwenda kuongeza kasi kwenye safu yao ya ushambuliaji kwa sababu kuna wachezaji wao wengi watarejea kwenye timu zao baada ya mkopo kumalizika.

 

 Mmoja wa wadau wa soka aliye karibu na KMC alisema: “Sheva anasubiri kutambulishwa wakati wowote na KMC kwa sababu mazungumzo baina yao yanakwenda vizuri kabisa.”

 

Alipotafutwa Msemaji wa KMC, Christina Mwagala alisema: “Sisi hatusajili mitandaoni, wachezaji ambao tutamalizana nao tutawatangaza pale kila kitu kikienda sawa.”

 

Sheva alikosa nafasi ya kucheza msimu uliopita, baada ya mwaka wake wa kwanza Simba akitokea Lipuli kwenda vizuri, lakini majeraha yalimuweka nje kwa muda mrefu na kufanya apoteze nafasi.


Chanzo:Championi

KUUZWA KWA CHAMA NA LUIS..EDO KUMWEMBE AFUNGUKA HAYA..ASEMA SIMBA NI TIMU NDOGO HAO YANGA HAWATANII..HIVI NDIVYO WALIVYOTEKETEZA KARIBU MILIONI 100 KISA MORRISON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply