News

CRISTIANO RONALDO:REKODI YANGA NA REAL MADRID IMEANDIKWA

admin August 18, 2021 5:43 am


MSHAMBULIAJI, Cristiano Ronaldo amesema kuwa kwa sasa habari yake ndani ya Real Madrid imeshaandikwa jambo ambalo linaleta ugumu kwa nyota huyo kuweza kurejea hapo kwa mara nyingine.

Nyota huyo alikuwa anatajwa kurejea Real Madrid inayotumia Uwanja wa Bernabeu na mkataba wake ndani ya Klabu ya Juventus ya Italia umebakisha miezi 12 na hajawaambia mabosi wake kwamba anahitaji kuondoka hapo.

Akiwa na umri wa miaka 36 bado amekuwa na uwezo mkubwa ndani ya uwanja jambo linalozivutia timu nyingi na iliwahi kuelezwa kuwa Manchester United nao pia wanahitaji saini yake ili kumrejesha kwenye timu hiyo.

Pia hata Juventus wenyewe wameeleza kwamba hawajapokea ofa yoyote kutoka timu yoyote ambayo inamhitaji nyota huyo kwa ajili ya kupata saini yake.

Nyota huyo amesema kuwa mengi ambayo yanaendelea juu yake hasa kwenye vyombo vya habari ni tetesi na wapo ambao wanashindwa kumuheshimu jambo ambalo halipendi kuona likitokea.

“Mambo yangu kuhusu Real Madrid tayari yameshaandikwa na ni rekodi. Muda wa miaka nane ambao nimefanya kazi hapo kuna namba na maneno pia ikiwa ni mataji, rekodi na habari. Ninajua kwamba mashabiki walivyo nami ninawaheshimu pia,” .

AZAM FC SERA YAO MPYA NI MWENDO WA KIMYAKIMYA SIMBA KUYAKOSA MABAO 42 NDANI YA LIGI KUU BARA MAZIMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply