kimataifa

MANCHESTER CITY KUMCHUKUA RONALDO MAZIMA

admin August 27, 2021 3:43 am


MANCHESTER City wanapewa nafasi ya kuipata saini ya nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo kwa kuwa mabosi wake wa sasa wanahitaji kumuuza kutokana na kile kinachoelezwa kutumia gharama kubwa kwa ajili yake kwa malipo ndani ya wiki moja.

Ikiwa Juventus wataweza kumuuza nyota huyo wanaweza kupunguza matumizi makubwa ya mkwanja ambao unatajwa kuwa ni Euro 500,000 kwa wiki ambao ni kwa ajili ya malipo ya mchezaji huyo ambayo wanamlipa ukijumlisha na kodi.

City wanatajwa kuwa wanahitaji kuipata saini ya mshambuliaji huyo raia wa Ureno mwenye miaka 36 ili akaungane nao msimu mpya na wapo tayari kumpa dili la miaka miwili kwa mujibu wa Sky Sports.

Dili la City kumpata Harry Kane tayari limebuma baada ya nyota mwenyewe kuthibitisha kwamba atabaki ndani ya Tottenham hivyo City wanahamishia nguvu kwa Ronaldo ili awe ndani ya Uwanja wa Etihad.

Kwa sasa  Cristiano Ronaldo mkataba wake ndani ya kikosi hicho cha Juventus umebakisha mwaka mmoja lakini kuna uwezekano mkubwa wa yeye kuondoka kwa kuwa mabosi wameamua hivyo huenda ikawa hivyo.

Jorge Mendes, wakala wa mchezaji huyo  yupo kwenye harakati za kumtafutia mteja wake timu mpya na ni timu mbili zinapewa nafasi ya kupata saini yake PSG na Man City kwa kuwa hizi amekuwa katika mazungumzo nazo.

BAADA YA MANARA KUHAMIA YANGA…KADUGUDA AIBUKA NA HILI..AMTAJA MO DEWJI NYOTA AZAM FC KUIBUKIA KMC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply