news

DODOMA JIJI KAZIKAZI MOROGORO

admin September 7, 2021 5:43 am


KIKOSI cha mabosi wa Zabibu na wakulima wa zao hilo, Dodoma Jiji kimejiwekea chimbo kwa sasa Morogoro wengi wanapenda kupaita mji kasoro bahari.

Chini ya Kocha Mkuu, Mbwana Makata ambaye ni mzawa kimeendelea na maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 unaoatrajiwa kuanza Septemba 29 na mchezo wa ufunguzi ambao ni wa Ngao ya Jamii kati ya Simba v Yanga unatarajiwa kuchezwa Septemba 25, Uwanja wa Mkapa.

Kikosi hicho kilimaliza msimu kikiwa nafasi ya 8 na kilikusanya pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 34.

Ikumbukwe kwamba ulikuwa ni msimu wake wa kwanza kushiriki Ligi Kuu Bara na kiliweza kuonyesha ushindani mkubwa.

Ni Gwambina na Ihefu ambazo zilipanda pamoja na Dodoma Jiji msimu wa 2020/21 ila kwa sasa hizi mbili zitashiriki Ligi Daraja la Kwanza ambayo kwa sasa inaitwa Championship baada ya kukwama kwenda na kasi ya Ligi Kuu Bara.


DOZI YA YANGA,KUTWA MARA MBILI SIKU 10 ZA MICHEZO YA KIMATAIFA KUTAMATIKA WIKI HII

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply