kimataifa

ISHU YA MECHI KUAHIRISHWA, MESSI AMECHUKIA KWELIKWELI

admin September 7, 2021 4:43 am


BAADA ya mchezo kati ya Brazil na Argentina kupigwa stop juzi, nahodha wa Argentina,  Lionel Messi amechukizwa na kitendo hicho akidai kuwa haikuwa sahihi kwani walikuwa hapo kwa siku tatu.

Mchezo huo ulipigwa stop baada ya Ofisa mmoja wa afya wa Brazil kuingia uwanjani wakati mchezo ukiendelea na kutaka baadhi ya wachezaji wa Argentina waondolewe uwanjani.

Wachezaji ambao walitakiwa kuondolewa Uwanjani ni Emiliano Martinez, Cristiano Romero, Gio Lo Celso ambao wanacheza Premier League sababu wamesafiri kutoka England na hawakukaa karantini kwa muda wa siku 14 kama ambavyo sheria za Brazil zinasema.

Messi amesema:”Walipaswa kutuondoa nchini mwao siku tatu baada ya kuwasili lakini kwa nini wasubiri mpaka mchezo uanze ndipo wafanye hivyo?

“Wangetuambia mapema hili tungejua ni namna gani mambo yangekuwa hivi watu wanatuangalia,”.


JESSE ACHEKELEA KUFUNGA TIMU YA TAIFA MUGALU ATUMA UJUMBE HUU KWA MASHABIKI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply