News

DUH! KUMBE HAJI MANARA HAJAWAHI KUWA SIMBA…ADAI ALIKUWA ANADANGANYA

admin September 9, 2021 2:43 pm

HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa hajawahi kuwa Simba zaidi yeye alikuwa Yanga katika maisha yake yote.

Kwa sasa Manara ni Ofisa Habari wa Yanga ambapo aliibuka huko muda mfupi baada ya kubwaga manyanga ndani ya Klabu ya Simba na huko alikuwa ni Ofisa Habari alidumu kwa muda wa miaka 6.

Manara amesema:”Nazungumzia fact, mimi sijawahi kuwa Simba na mimi sio Simba zaidi mimi ni Yanga.

“Moja ya kazi kubwa niliyoifanya labda ni kuonesha ukubwa feki hiyo dhambi niliitendea vibaya sana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nipo tayari kuhukumiwa hata gerezani kwa kufanya ulaghai wa kufix ukubwa ambao haupo.

Haji ameongeza kuwa Yanga ndio klabu yenye mataji mengi zaidi vinginevyo ni uongo ambao yeye mwenyewe hapo nyuma alishiriki kuupika.

Chanzo: E FM

LUIZ KUIBUKIA SERIE A BAADA YA SAMATTA KUUZWA TENA UBELIGIJI..EDO KUMWEMBE AFUNGUKA YA MOYONI…AMTAJA MSUVA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply