news

RUVU SHOOTING YATAMBIA USAJILI WAKE

admin September 26, 2021 2:43 pm


 MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting ameweka wazi kuwa msimu mpya wa 2021/22 watafanya vizuri kutokana na usajili ambao wameufanya.

Usiku wa kuamikia leo Ruvu Shooting walikuwa na jambo lao lililopewa jina la Usiku wa Ruvu Shooting na liliweza kufana kwa uzuri na wengi walihudhuria.

Akizungumza na Saleh Jembe, Masau amesema kuwa kwa namna ambavyo wamefanya usajili pamoja na maandalizi ambayo wameyafanya imani yao ni kupata matokeo chanya.

“Tumefanya usajili mzuri hilo lipo wazi na kila mmoja anatambua kwamba Ruvu Shooting ni sehemu ambayo ina wachezaji wengi wazawa na wapambanaji muda wote.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita, hilo lipo wazi na wachezaji wetu wote hilo wanalitambua ni suala la muda tu,” amesema Masau.

Msimu uliopita Ruvu Shooting ilimaliza ikiwa nafasi ya 11 na pointi zake zilikuwa ni 41 kibindoni.

HAPA NDIPO SIMBA WALIPOTEANA,KIMATAIFA MIPANGO INAHITAJIKA ARSENAL GARI LIMEWAKA HUKO,YAICHAPA TOTTENHAM

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply