kimataifa

SOLSKJAER AMKINGIA KIFUA BRUNO FERNANDES

admin September 26, 2021 11:43 am


LICHA ya nyota wa Manchester United,  Bruno Fernandes kukosa penalti katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Aston Villa bado mabosi wa timu hiyo wamesema wapo pamoja naye huku Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer akitaja sababu za nyota huyo kupiga penalti. 

Wakiwa Uwanja wa Old Trafford, United ilikubali kunyooshwa kwa bao 1-0 ambalo lilijazwa kimiani na Kortney Hause dakika ya 88 na kuifanya timu hiyo kusepa na pointi tatu mazima.

Ilikuwa dakika ya 90 ambapo United ikiwa na nyota wake mtambo wa mabao Cristiano Ronaldo ilipata penalti na jukumu la kupiga likawa miguuni mwa Bruno.

Shuti lake kali alilopiga lilikwenda juu ya lango na kuifanya United kushindwa kusepa na pointi hata moja jambo ambalo limewaumiza mashabiki wa timu hiyo.

Solksjaer amesema:”Suala la kupoteza sio zuri lakini kufungwa kwetu maana yake ni kwamba tunapaswa kuinuka na kufanya vizuri kwa mechi zijazo.

“Kwa upande wa upigaji wa penalti ni jambo ambalo linapangwa kabla ya mchezo na sio wakati wa mchezo hivyo kwa kilichotokea hakuna ambaye alikusudia ni sehemu ya mchezo,”.


EXCLUSIVE:KMC YAZIWEKA KANDO SIMBA V YANGA, HESABU ZAKE HIZI HAPA KUMBE MUUAJI WA SIMBA ALIPANIA KUFANYA HIVYO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply