KMC FC

KMC YATAMBA KUENDELEZA NA PIRA SPANA,PIRA KODI

admin September 27, 2021 2:43 pm


 UONGOZI  wa KMC umeweka wazi kuwa unahitaji kufanya vizuri kwenye mechi zake zote za Ligi Kuu Bara na itaanza kufanya hivyo mbele ya Polisi Tanzania.

Septemba 29 KMC itakuwa na kazi mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi na leo kikosi kinatarajiwa kuanza safari kuibukia huko Moshi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema kuwa wanatambua kwamba ligi inaanza na wana malengo ya kufanya vizuri hivyo wataanza kufanya hivyo mbele ya Polisi Tanzania.

“Kuanza kwa ligi kwetu sisi ni maandalizi na mwanzo mzuri ni jambo ambalo tunalihitaji hivyo tutaanza kufanya mbele ya Polisi Tanzania, maandalizi ambayo tumeyafanya ni makubwa na tunaamini tutafanya vizuri.

“Kikubwa mashabiki wazidi kuwa nasi hatutawaangusha na tutaendelea na pira letu lile, pira spana na pira kodi na kwa usajili ambao tumefanya ni moto wa kuotea mbali,” alisema.

Nyota ambao ni wapya ndani ya KMC ni pamoja na Farokh Shikalo ambaye alikuwa anakipiga Yanga pamoja na Miraj Athuman aliyekuwa anacheza Simba.

HAJI MANARA TAMBO KAMA ZOTE, NGUVU ZAO SASA NI KWENYE LIGI KUU BARA ZAWADI YA MAYELE KUTOKA SIMBA, MASHABIKI KUMBE WALISUSA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply