News

KAPOMBE KUUKOSA MCHEZO WA KESHO..SABABU HIZI HAPA…MATOLA ATOA KAULI

admin September 30, 2021 7:00 pm


Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe ndiye mchezaji pekee kati ya 23 waliopo kikosini ambaye atakosekana katika mchezo wa pili wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa kesho Uwanja wa Jamhuri saa 10 jioni.

Kapombe aliumia katika mchezo wetu wa kwanza wa ligi dhidi ya Biashara United ambapo alishindwa kuendelea na mechi kipindi cha pili akafanyiwa mabadiliko.

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema ukimuacha Kapombe wachezaji wengine wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho ambao tunaamini utakuwa mgumu.

“Tunahitaji alama tatu kwenye mchezo wa kesho kutokana na matokeo ya mechi zetu tatu za zilizopita ili kurudisha ari kikosini pamoja imani na hamasa kwa mashabiki.

“Maandalizi yamekamilika wachezaji wako tayari isipokuwa tutamkosa Kapombe kutokana na kuwa majeruhi. Tunafahamu ligi ni ngumu hasa mechi za ugenini kutokana na aina za viwanja lakini tupo kamili na lengo ni moja kupata alama tatu,” amesema Matola.

MZUNGUKO WA KWANZA UMEACHA REKODI HIZI BONGO MKANDALA ATUMA UJUMBE HUU KWA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply