news

FT: SIMBA 2-1 GEITA GOLD….BANDA AFUNGUA UFUNGUA UKURASA WA MABAO..SIMBA IKIPONEA CHUPUCHUPU….

admin December 1, 2021 6:29 pm


Winga Peter Banda amefunga bao lake la kwanza la mashindano akiwa na kikosi chetu katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Geita Gold uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo.

Banda alitupatia bao hilo dakika ya tisa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kibu Denis kutoka upande wa kulia.

Baada ya bao hilo Geita walikuja juu kutaka kusawazisha lakini safu yetu ya ulinzi iliyokuwa chini na Kennedy Juma na Joash Onyango ilikuwa makini.

Mzamiru Yassin aliipatia Simba SC bao la pili dakika ya 56 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Bernard Morrison sekunde chache baada ya kuingia kutoka benchi.

Dakika 66 Juma Mahadhi aliipatia Geita bao la kwanza kufuatia walinzi wetu wa kati kuzembea kuondoa hatari.

Kocha Pablo Franco aliwaingiza Bernard Morrison, Mzamiru Yassin, Erasto Nyoni, Medie Kagere na Pascal Wawa kuchukua nafasi za Ibrahim Ajibu, Rally Bwalya, John Bocco, Banda na Kibu.

Matokeo haya yameifanya Simba SC kufikisha alama 17 baada ya kucheza mechi saba tukishinda mitano na sare mbili.

AJIBU, BANDA NA GADIEL MICHAEL WAANZA DHIDI YA GEITA GOLD..KIKOSI KAMILI HIKI HAPA… KUELEKEA DABI…NABI ALINASA FAILI LA PABLO..MAYELE AITAJA SIMBA…SPOTI XTRA LEO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply