news

KARIAKOO DABI: SIMBA YAIWAHI YANGA TAIFA…YANGA WAINYATIA NYUMANYUMA KWA DAKIKA TATU…

admin December 11, 2021 1:25 pm


KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Kati ya Simba na Yanga utakaochezwa saa 11:00 za jioni, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa wenyeji Simba ndio wamekuwa wakwanza kufika uwanjani hapo.

Kikosi cha wenyeji Simba kimewasili Uwanjani hapo saa 9:27 Alasiri na basi lao kubwa na dakika tatu  baadae Yanga ambao ni wageni wa mchezo huo waliwasili Uwanjani.

Baada ya kufika timu zote mbili ziliingia Uwanjani kupitia geti kubwa la Uwanja wa Mkapa  na kupitiliza hadi katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Wakati Simba na Yanga zikipita kwenye barabara za nje ya Uwanja wa Mkapa, kuingia ndani mashabiki wa timu hizo waliopo nje walizishangilia kwa sauti kubwa.

Mechi hiyo ni ya kwanza kuwakutanisha watani hao wa jadi katika ligi msimu huu lakini Septemba 25, mwaka huu zilikutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii na Yanga kuibuka na Ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Fiston Mayele.

DAKIKA KADHAA KABLA YA KARIAKOO DABI…BARBARA AIBUKA NA JIPYA KUHUSU MORRISON NA MKUDE… KARIAKOO DABI: HIVI HAPA VIKOSI VYA TIMU ZOTE MBILI…..BWALYA NA MUKOKO ‘OUT’..KAGERE, MAYELE KAMA KAWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply