News

KUHUSU ISHU YA KUMZUIA WAWA ASINGIE UWANJANI…PABLO AVUNJA UKIMYA…ATOA LAWAMA…

admin December 26, 2021 9:00 am


PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kilichotokea kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC ni kutoelewana na mwamuzi.

Juzi Pablo akiwa benchi alionekana kumzuia Pascal Wawa asiweze kuingia kuendelea kutimiza majukumu yake.

Kwenye mchezo huo ubao wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ulisoma KMC 1-4 Simba na kuiwafanya mabingwa hao watetezi kusepa na pointi tatu.

Pablo amesema:”Suala hili halikuhitaji ufafanuzi lakini ni jambo ambalo limetokea katika mchezo wetu hasa katika upande wa mabadiliko.

“Jambo lililotokea naweza kusema ni kushindwa kuwa na mawasiliano mazuri na mwamuzi katika suala la mabadiliko lakini mambo mengine yanakwenda sawa.

“Sina tatizo na mchezaji Wawa kwa kuwa ni mchezaji mzuri na anatimiza majukumu yake,” amesema Pablo.

VIGOGO SIMBA WAAMUA KUIFANYIA UMAFYA YANGA KWENYE ISHU YA CHAMA…WAIBUKA NA JIPYA HILI.. KUHUSU ISHU YAKE YA KUJA YANGA…CHIKO USHINDI AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA A-Z MCHONGO ULIVYO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply