News

WAKATI YANGA WAKIMTAKA NGUSHI…MBEYA KWANZA WAIBUKA NA HILI…

admin December 27, 2021 7:39 am


WAKATI kukiwepo na tetesi za Yanga kumuhitaji straika Chrispin Ngushi, mabosi wa straika huyo Mbeya Kwanza wameibuka na kubainisha kuwa wapo tayari kumuachia nyota huyo kutua Jangwani.

Ngushi amekuwa na msimu mzuri hadi sasa akiwa na Mbeya Kwanza ambapo ameweka kambani mabao matatu na asisti moja.

Akizungumza na gazeti la  Championi Jumamosi, Mwenyekiti wa Mbeya Kwanza, Mohammed Mashango alisema kuwa endapo Yanga watakuwa tayari kwa ajili ya mazungumzo basi wao kama timu watamuachia mchezaji huyo.

“Hadi sasa bado hatujapata ofa yoyote kutoka kwa Yanga lakini tumekua tukisikia kuwa wanamuhitaji lakini bado hawajafika kwetu kama wakija tukafanya mazungumzo na tukafikia makubaliano mazuri basi kila kitu kitakuwa wazi.

“Sisi kama timu tupo tayari kumuachia Chrispin kwenda Yanga kwani lengo letu ni kuona vijana wetu wanakuza vipaji, kwa hiyo hatutakuwa na pingamizi kwenye jambo hilo,” alisema Mashango.

IMEFICHUKAA…HIVI NDIVYO USAJILI WA  ‘SURE  BOY’ ULIVYOIKAMUA YANGA MAMILIONI YA PESA… HIVI NDIVYO DILI LA MAKUSU KUTUA YANGA LILIPOFIKIA…UONGOZI BAADA YA KUTONYWA..WAMFUNGIA VIOO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply