News

KUHUSU ISHU YA PETER BANDA KUTIMKIA SAUDI ARABIA…UONGOZI SIMBA WATOA NENO..BARUA YAPOKELEWA…

admin December 30, 2021 5:00 pm


STAA wa Simba, Peter Banda ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi ‘The Flames’ kuelekea Afcon 2021 huko nchini Cameroon.

Tayari kikosi hicho cha Malawi kimesafiri kuelekea nchini Saudi Arabia ambako kitaweka kambi yao fupi ya mwisho kabla ya kuelekea Cameroon.

Banda bado yupo nchini ambaye juzi alikuwa katika kikosi cha timu mkoani Tabora kilichocheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC FC.

Shirikisho la Soka la Malawi limetuma barua pepe kwa uongozi wa Simba ya kuomba umruhusu kiungo huyo kujiunga na kambi yao ya Saudi Arabia.

Malawi wameuomba uongozi wa Simba kumruhusu kuondoka nchini leo Jumatatu tayari kwa kujiunga na kikosi cha timu hiyo.

Akizungumzia hilo, Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ally Shatry alisema kuwa “Tumepokea barua ya kumruhusu Banda kwenda kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya Malawi, hivyo haraka tutamruhusu kwa ajili ya kujiunga na kikosi hicho.”

TAA YA KIJANI YAMWAKIA KIBU DENIS….KUPIGWA BEI ULAYA …MAGORI AFUNGUKA DILI LOTE A-Z… BAADA YA WAWILI..NABI KUFUNGA USAJILI NA MASHINE MBILI MATATA..SIMBA YAMTISHA IBENGE….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply