News

SAKHO AFUNGUKA KUHUSU BAO ALILOWAFUNGA WAIVORY…ADAI LINAMAANA HII…HAKUWA NA BAHATI….

admin February 16, 2022 3:00 pm


LILE bao la kideo ambalo alifunga nyota wa Simba, Pape Ousmane Sakho kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast unaambiwa haikuwa bahati mbaya kwa Msenegal huyo.

Wakati Simba ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo huo, Kocha wa Simba Pablo Franco alimuandaa Sakho.

Katika mazoezi hayo karibu wiki nzima, Sakho alionekana kufanya vizuri na mara kadhaa licha ya kufunga mabao mengi makali alifanya majaribio ya kufunga kwa kujibetua ‘tikitaka’ lakini hakuwa na bahati ya kupachika bao, alifanya hivyo siku ya Alhamisi kwenye Uwanja wao wa mazoezi wa Mo Simba Arena. Sakho alisema aina ya ufungaji wake amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara akiwa na timu mbalimbali alizocheza kwao Senegal.

“Bao lina maana kubwa kwa timu kwani tulihitaji kuongoza kipindi cha kwanza na niliitumia vizuri kazi waliyoifanya wachezaji wenzangu hadi kuwa mtu wa mwisho kuweka mpira kambani,” alisema Sakho na kuongeza;

“Simba tunahitaji kufanya vizuri katika mashindano haya na hicho ndio kikubwa tumeingia nacho wachezaji wote ndio maana nilicheza kwa kujituma zaidi.”

PAMOJA NA KUICHAPA ASEC JUZI…PABLO ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU KAGERE…ZIMBWE JR NA NYONI WATIA NENO… BAADA YA KUJITOA LIGI KUU…GSM AFANYA KUFRU YANGA…APITA NJIA ILE ILE YA MO DEWJI SIMBA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply