News

DALALI AINGILIA KATI ISHU YA UBINGWA SIMBA…ADAI WAMESHIKIWA NAFASI …ATOA ONYO HILI…

admin February 17, 2022 3:11 pm


LICHA ya Yanga kuongoza Ligi Kuu Bara kwa tofauti ya alama tano, aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali, amesema kuwa Yanga imewashikia kwa muda tu nafasi yao.

Yanga kwa sasa wako kileleni mwa ligi kuu wakiwa na pointi 36 baada ya kushuka dimbani mara 14 ambapo wameshinda mechi 11 na sare tatu.

Simba wao wamecheza mechi 15, wameshinda tisa, sare nne na kupoteza mbili wako nafasi ya pili na alama zao 31.

Dalali alisema kuwa: “Kuhusu ubingwa wa Ligi Kuu Bara hilo halina ubishi wale wenzetu wametushikia nafasi yetu na muda utakapowadia tunakwenda kuwashusha na safari ya ubingwa itaanzia hapo, kikubwa tuwe wamoja tusitengeneze makundi ambayo yatakuja kutuvuruga na tukatoka kwenye malengo yetu.”

KWA TAARIFA YAKO…HII HAPA REKODI ALIYOWEKA BOCCO BAADA YA KUFUNGA GOLI MBILI JANA.. BAADA YA KUPIGWA 7-0 JANA..MASAU BWIRE AIBUKA NA SABABU HIZI…ADAI WANAMAJONZI YA MSIBA WA SONSO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply