News

KISA MOLOKO NA USHINDI…NABI AKUNJA USO…KISHA AKAFUNGUKA HAYA…HANA JINSI YANI…

admin February 19, 2022 3:21 pm


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kuwa kukosekana kwa wachezaji wake zaidi ya saba katika kikosi chake, kunamvurugia mipango ya ushindi kuelekea michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Hiyo ni baada ya kuongezeka kwa majeruhi katika kikosi chake ambao ni Mkongomani, Jesus Moloko aliyeshindwa kumalizia mchezo wa FA dhidi ya Biashara United uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Yanga katika mchezo huo iliwakosa wachezaji saba, kati ya hao ni kutokana na majeraha ambao ni Yacouba Songne, Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Chico Ushindi, Denis Nkane, Chrispin Ngushi na Dickson Job anayetumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu.

Nabi alisema kuwa katika timu wanapokosekana wachezaji zaidi ya saba kunaharibu mipango ya kiufundi ya kocha katika kupata ushindi.

Nabi alisema kuwa kikosi chake kinakabiliwa na wachezaji wengi majeruhi, hadi unafikia wakati analazimika kuwatumia majeruhi kama ilivyokuwa kwa Moloko ambaye alimtumia akiwa ana majeraha katika mchezo.

BAADA YA KUSHTUKIA SIMBA WAKO NYUMA YAO KWA POINTI 5…NABI AFIKIRIAA WEE…KISHA AKATOA KAULI HII…. KISA KIFO CHA ALLY MTONI ‘SONSO…EZEKIEL KAMWAGA AWAVAA RUVU SHOOTING…AFICHUA UZEMBE ULIVYOKUWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply