News

WAKATI MTIBWA WAKITAMBIA UWANJA WA MANUNGU…MANARA AIBUKA NA HILI…ATOA MSIMAMO WA YANGA….

admin February 23, 2022 5:40 am


MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amesema mchezo wao wa leo Februari 23 dhidi ya Mtibwa Sugar wanahitaji pointi tatu na sio kitu kingine.

Mtibwa na Yanga wanacheza leo saa 10:00  katika Uwanja wa Manungu uliopo Turiani, Manungu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazoezi kumalizika, Manara amesema mchezo huo utakuwa mgumu lakini watatoka na pointi tatu.

Manara amesema Mtibwa wana timu nzuri na wachezaji wenye uzoefu huku kila mmoja akitaka kujitangaza.

“Kikosi cha Mtibwa kipo vizuri na wanafahamu vizuri Ligi, sisi tupo tayari kwa ajili ya mchezo na kuchukua pointi tatu,” amesema Manara na kuongeza;

“Hizi ni mbio na bado zinaendelea kwahiyo muhimu kwanza kuchukua pointi tatu.”

Yanga wanaingia kwenye mchezo huo huku wakiwa na kumbukumbu ya kuifunga Mtibwa 4-2 mchezo uliochezwa 1992 katika uwanja wa Manungu.

SIMBA WAZIDI KUFANYA MAKUBWA…WAMSHUSHA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA QATAR…KUWA MSAIDIZI WA PABLO… PABLO ALIA WACHEZAJI WA SIMBA KUKOSA PUMZI NIGER…ADAI HALI YA HEWA NI TATIZO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply