KMC FC

KAMA ULIDHANI KMC IMEANZA KUKATA PUMZI….ILA SAHAU…WAZIPIGIA HONI POINT 6 ZA KANDA YA ZIWA…

admin April 12, 2022 11:24 pm


Kikosi cha wachezaji 24, Benchi la ufundi pamoja na viongozi wa klabu ya KMC FC kitaondoka Jijini Dar es Salaam kesho kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumapili Aprili 17, 2022. Uwanja wa Kaitaba.

Mbali na mchezo huo dhidi ya Kagera, KMC FC pia itakuwa na mchezo mwingine wa ugenini dhidi ya Geita Gold FC utakaochezwa Aprili 23 mchezo huu utapigwa katika uwanja wa Nyankumbu.

Kuelekea katika michezo hiyo miwili ya kanda ya ziwa Afisa Habari wa klabu hiyo Christina Mwagala amesema malengo yao ni kushinda michezo yote hiyo miwili na kuvuna alama zote 6.

“KMC tunakwenda Kanda ya ziwa kesho, kutafuta alama sita kutoka kwenye Timu ya Kagera Sugar pamoja na Geita, tunafahamu kuwa Timu hizo ni nzuri na zimekuwa na matokeo mazuri kwenye michezo yao, lakini hiyo haituzuii Manispaa ya Kinondoni tukashindwa kupata alama zote kwasababu zipo ndani ya uwezo wetu.’’ Amesema Mwagala

 KMC ipo nafasi ya 9 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 23 katika michezo 19, na imeshinda michezo miwili tu kwenye michezo mitano ya mwisho kwenye ligi wamefungwa michezo miwili na sare mchezo mmoja

SIMBA YASHUSHA PACHA WA INONGA…BOSI MSIMBAZI AKUBALI YAISHE KWA MAYELE….DALALI AOTA TANO…. KADUGUDA: – ‘KAMA INAHITAJIKA MTU AFE ILI TUWE MABINGWA ..NIPO TAYARI…NITAFUNGUA TAWI AKHERA…’

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply